Jumatano, 11 Machi 2015

KOCHA ADOLFU RICHARD ASITISHIWA MKATABA WAKE NA TIMU YA POLISI MORO.

Uwongozi wa timu ya soka ya Polisi Moro ya mkoani morogoro inayo shiriki ligi kuu tanzania bara, leo imemsitishia rasmi mkataba wake aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo ADOLFU RICHARD.Akizungumzia suala hilo kocha Adolfu alisema" amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makuwa na amekubaliana na maamuzi hayo kwa faida ya timu na jambo ambalo lilikuwa ndani ya mkataba wake na timu hiyo.Alisema sababu kubwa iliyo mfanya kocha huyo kusitishiwa mkataba wake ni kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michezo yake ya hivi karibuni baada ya timu ya Polisi moro kufungwa na timu ya Simba 1-0, kufungwa na Kagera sukari 2-1, na kufungwa na Mtibwa sukari bao 2-1 pamoja na kutoa suluu ya bila kufungana na timu ya Ruvu shooting katika uwanja wa jamuhuri morogoro".Baada ya matokeo hayo uwongozi  wa timu ya Polisi Moro ulimtaka kocha huyo kutoa maelezo juu ya matokeo hayo na ndipo ulipo amua kutoa maamuzi ya kumsitishia kocha huyo mkataba wake.
Kwa sasa timu hiyo inashikiriwa na kocha wake msaidizi JOHN TAMBA ikiwa na point 20.