Mabingwa wa mapinduzi cup,Simba sport club hapo kesho wanaingia dimbani kukipiga na timu ya Mtibwa sugar katika uwanja wa taifa jijini dar es samaal. Simba wanaingia dimbani hapo kesho wakiwa na rekodi ya kutoa sale ya bao 1-1 dhizi ya Mtibwa katika uwanja wa jamuhuri mjini morogoro, pila Simba ikafanikiwa kuutwaa ubingwa wa kombe la mapinduzi dhizi ya Mtibwa baada ya kuwatoa kwa njia ya penati. Simba iliyo na makazi yake mtaa msimbazi kariakoo jijini dar es salaam inaingia dimbani kesho baada ya kumfunga mtani wake wa jadi wana wa jangwani Yanga bao 1-0 wiki iliyo pita, bao ambalo lilifungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi katika uwanja wa taifa.
Pia wakata miwa wa Turiani morogoro wamekwisha wasili jijini dar es salaam leo majira ya saa tisa mchana tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo wa kesho.
Mtibwa ikiwa chini ya kocha wake mkuu MEKI MEXIME na msaidizi wake Zuberi Katwila wakiwa tayari kabisa kukipiga na mnyama huyo hapo kesho majira ya saa 10:00 jioni.
Jumamosi, 14 Machi 2015
SIMBA USO KWA USO KESHO DHIDI YA MTIBWA SUGAR.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)