Jumapili, 15 Machi 2015

KIGAMBONI SOCCER ACADEMY; BADO AZAM.

Ni kauli za kocha mkuu bwn Mohamedi na kocha msaidizi bwn Kiiza walisema hayo baada ya timu yao ya Kigamboni Soccer Academy kuebuka na ushindi mnono walio upata dhidi ya timu ya Mbutu FC wa mabao 4-1. Timu ya Kigamboni Soccer Academy ilijipatia bao lake la kwanza ktk dakika ya kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake mashuhuli Davidy, licha ya kupoteza nafasi nyingi  timu ya Kigamboni Soccer ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Davidy ambapo lilikuwa bao lake la pili katika mchezo huo. Licha ya timu hiyo ya Mbutu kupata nguvu  na kujipatia bao lake la kufutia machozi ndipo kiungo mkabaji wa Kigamboni Soccer Academy pia ni mchezaji wa timu ya Majimaji ya songea iliyo fanikiwa kupanda daraja katika ligi kuu akitokea kituo hicho cha vipaji  Hassan akaiandikia timu yake bao la tatu lililo dumu kipindi chote cha kwanza, hadi kufikia mapumziko Kigamboni Soccer Academy ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1. Baada ya mapumziko mshambuliaji hatari na mwenye kiu ya magoli Bashiru alizidi kuwakatisha tamaa timu ya Mbutu kwa kuzidi kukandamiza msumali wa moto katika goli la Mbutu na kuzidi kuongeza ushindi mnono kwa timu yake. Hadi dakika 90 zinamalizika timu ya Kigambini Soccer Academy ilitoka kifua mbele kwa mabao 4-1 dhidi ya Mbutu. Nao viongozi wa Kigamboni Soccer walisema kuwa ushindi huo ni salamu tosha kwa timu ya AZAM U20 ambapo wanatarajia kucheza na timu ya Kigamboni Soccer Academy ambao wanatarajia kucheza siku chache za hivi karibuni.