Timu ya soccer ya Kigamboni Academy yenye makazi yake maeneo ya kigamboni jijini dar es salaam, imejipanga vyema kucheza mchezo wa kihistoria hapo kesho katika mchezo wa kirafiki utakao pigwa dhidi ya MBUTU FC ya nje kidogo ya maeneo ya kigamboni katika uwanja wa shule ya msingi Kigamboni.
Licha ya timu ya MBUTU kuifunga timu ya KIGAMBONI SOCCER mabao 3-2 majuma kadhaa yaliyo pita, lakini timu hiyo imejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo hapo kesho. Nae kocha mkuu wa KIGAMBONI SOCCER ACADEMY Bwn Mohamed amethibitisha kuwa timu yake iko vizuru kwani ilitoka kucheza mchezo wa kirafiki wiki iliyo pita na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya timu ya BODABODA FC.Amesema hayo kocha huyo bwana Mohamedi akiwa mazoezini katika uwanja wao wa shule ya msingi kigamboni kwamba" timu yake imekuwa katika mazoezi magumu sana wiki hii na sio tu kwa sababu ya mchezo wao wa kesho ila pia inajiandaa na mchezo mkali dhidi ya wapinzani wao wakali AZAM FC U20 pamoja mchezo wao wa nusu fainal.
Ijumaa, 13 Machi 2015
KIGAMBONI SOCCER ACADEMY YAJIPANGA KULIPIZA KISASI KESHO.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)