Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC jana imezidi kujiongezea pointi 3 muhumu baada kuichapa timu ya Mtibwa SC bao 1-0 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.Timu hizo zilicheza katika kipindi cha kwanza hadi kwenda mapumziko bila kufungana. Zilipo ingia kipindi cha pili timu hizo zilianza kwa kushambuliana na baadae dakika chache kabla ya mpira kumalizika mnamo dakika ya 92 ya nyongeza baada ya kuisha kwa dakika 90,timu ya Simba ilijipatia bao lake la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa na raia wa Uganda EMMANUEL OKWI. Okwi aliifungia timu yake dakika ya 92 dakika 3 kabla ya mchezo kumalizika na kuwafanywa wapinzani wao Mtibwa kubaki wameduwaa na kumuona kama mwiba mchungu na kuwafanya mashabiki wao kutoka na furaha uwanjani hapo.Nayo timu ya Mtibwa sukari ilimpongeza Okwi lakini haikufurahishwa na maamuzi ya marefarii na kusema hawakutenda haki katika mchezo huo kwani wamekuwa wakiibeba sana timu ya Simba.
Jumapili, 15 Machi 2015
KIGAMBONI SOCCER ACADEMY; BADO AZAM.
Ni kauli za kocha mkuu bwn Mohamedi na kocha msaidizi bwn Kiiza walisema hayo baada ya timu yao ya Kigamboni Soccer Academy kuebuka na ushindi mnono walio upata dhidi ya timu ya Mbutu FC wa mabao 4-1. Timu ya Kigamboni Soccer Academy ilijipatia bao lake la kwanza ktk dakika ya kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake mashuhuli Davidy, licha ya kupoteza nafasi nyingi timu ya Kigamboni Soccer ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Davidy ambapo lilikuwa bao lake la pili katika mchezo huo. Licha ya timu hiyo ya Mbutu kupata nguvu na kujipatia bao lake la kufutia machozi ndipo kiungo mkabaji wa Kigamboni Soccer Academy pia ni mchezaji wa timu ya Majimaji ya songea iliyo fanikiwa kupanda daraja katika ligi kuu akitokea kituo hicho cha vipaji Hassan akaiandikia timu yake bao la tatu lililo dumu kipindi chote cha kwanza, hadi kufikia mapumziko Kigamboni Soccer Academy ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1. Baada ya mapumziko mshambuliaji hatari na mwenye kiu ya magoli Bashiru alizidi kuwakatisha tamaa timu ya Mbutu kwa kuzidi kukandamiza msumali wa moto katika goli la Mbutu na kuzidi kuongeza ushindi mnono kwa timu yake. Hadi dakika 90 zinamalizika timu ya Kigambini Soccer Academy ilitoka kifua mbele kwa mabao 4-1 dhidi ya Mbutu. Nao viongozi wa Kigamboni Soccer walisema kuwa ushindi huo ni salamu tosha kwa timu ya AZAM U20 ambapo wanatarajia kucheza na timu ya Kigamboni Soccer Academy ambao wanatarajia kucheza siku chache za hivi karibuni.