Jumapili, 15 Machi 2015

MSIMBAZI LEO NI SHEREHE, OKWI MWIBA MKALI.

Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC jana imezidi kujiongezea pointi 3 muhumu baada kuichapa timu ya Mtibwa SC bao 1-0 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.Timu hizo zilicheza katika kipindi cha kwanza hadi kwenda mapumziko bila kufungana. Zilipo ingia kipindi cha pili timu hizo zilianza kwa kushambuliana na baadae dakika chache kabla ya mpira kumalizika mnamo dakika ya 92 ya nyongeza baada ya kuisha kwa dakika 90,timu ya Simba ilijipatia bao lake la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa na raia wa Uganda EMMANUEL OKWI. Okwi aliifungia timu yake dakika ya 92 dakika 3 kabla ya mchezo kumalizika na kuwafanywa wapinzani wao Mtibwa kubaki wameduwaa na kumuona kama mwiba mchungu na kuwafanya mashabiki wao kutoka na furaha uwanjani hapo.Nayo timu ya Mtibwa sukari ilimpongeza Okwi lakini haikufurahishwa na maamuzi ya marefarii na kusema hawakutenda haki katika mchezo huo kwani wamekuwa wakiibeba sana timu ya Simba.

KIGAMBONI SOCCER ACADEMY; BADO AZAM.

Ni kauli za kocha mkuu bwn Mohamedi na kocha msaidizi bwn Kiiza walisema hayo baada ya timu yao ya Kigamboni Soccer Academy kuebuka na ushindi mnono walio upata dhidi ya timu ya Mbutu FC wa mabao 4-1. Timu ya Kigamboni Soccer Academy ilijipatia bao lake la kwanza ktk dakika ya kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake mashuhuli Davidy, licha ya kupoteza nafasi nyingi  timu ya Kigamboni Soccer ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Davidy ambapo lilikuwa bao lake la pili katika mchezo huo. Licha ya timu hiyo ya Mbutu kupata nguvu  na kujipatia bao lake la kufutia machozi ndipo kiungo mkabaji wa Kigamboni Soccer Academy pia ni mchezaji wa timu ya Majimaji ya songea iliyo fanikiwa kupanda daraja katika ligi kuu akitokea kituo hicho cha vipaji  Hassan akaiandikia timu yake bao la tatu lililo dumu kipindi chote cha kwanza, hadi kufikia mapumziko Kigamboni Soccer Academy ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1. Baada ya mapumziko mshambuliaji hatari na mwenye kiu ya magoli Bashiru alizidi kuwakatisha tamaa timu ya Mbutu kwa kuzidi kukandamiza msumali wa moto katika goli la Mbutu na kuzidi kuongeza ushindi mnono kwa timu yake. Hadi dakika 90 zinamalizika timu ya Kigambini Soccer Academy ilitoka kifua mbele kwa mabao 4-1 dhidi ya Mbutu. Nao viongozi wa Kigamboni Soccer walisema kuwa ushindi huo ni salamu tosha kwa timu ya AZAM U20 ambapo wanatarajia kucheza na timu ya Kigamboni Soccer Academy ambao wanatarajia kucheza siku chache za hivi karibuni.

Jumamosi, 14 Machi 2015

SIMBA USO KWA USO KESHO DHIDI YA MTIBWA SUGAR.

Mabingwa wa mapinduzi cup,Simba sport club hapo kesho wanaingia dimbani kukipiga na timu ya Mtibwa sugar katika uwanja wa taifa jijini dar es samaal.  Simba wanaingia dimbani hapo kesho wakiwa na rekodi ya kutoa sale ya bao  1-1 dhizi ya Mtibwa katika uwanja wa jamuhuri mjini morogoro, pila Simba ikafanikiwa kuutwaa ubingwa wa kombe la mapinduzi dhizi ya Mtibwa baada ya kuwatoa kwa njia ya penati. Simba iliyo na makazi yake mtaa msimbazi kariakoo jijini dar es salaam inaingia dimbani kesho baada ya kumfunga mtani wake wa jadi wana wa jangwani Yanga bao 1-0 wiki iliyo pita, bao ambalo lilifungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi katika uwanja wa taifa.
Pia wakata miwa wa Turiani morogoro wamekwisha wasili jijini dar es salaam leo majira ya saa tisa mchana tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo wa kesho.
Mtibwa ikiwa chini ya kocha wake mkuu MEKI MEXIME na msaidizi wake Zuberi Katwila wakiwa tayari kabisa kukipiga na mnyama huyo hapo kesho majira ya saa 10:00 jioni.

Ijumaa, 13 Machi 2015

KIGAMBONI SOCCER ACADEMY YAJIPANGA KULIPIZA KISASI KESHO.

Timu ya soccer ya Kigamboni Academy yenye makazi yake maeneo ya kigamboni jijini dar es salaam, imejipanga vyema kucheza mchezo wa kihistoria hapo kesho katika mchezo wa kirafiki utakao pigwa dhidi ya MBUTU FC ya nje kidogo ya maeneo ya kigamboni katika uwanja wa shule ya msingi Kigamboni.
Licha ya timu ya  MBUTU kuifunga timu ya KIGAMBONI SOCCER mabao 3-2 majuma kadhaa yaliyo pita, lakini timu hiyo imejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo hapo kesho. Nae kocha mkuu wa KIGAMBONI SOCCER ACADEMY Bwn Mohamed  amethibitisha kuwa timu yake iko vizuru kwani ilitoka kucheza mchezo wa kirafiki wiki iliyo pita na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 6-2  dhidi ya timu ya BODABODA FC.Amesema hayo kocha huyo bwana Mohamedi akiwa mazoezini katika uwanja wao wa shule ya msingi kigamboni kwamba" timu yake imekuwa katika mazoezi magumu sana wiki hii na sio tu kwa sababu ya mchezo wao wa kesho ila pia inajiandaa na mchezo mkali dhidi ya wapinzani wao wakali AZAM FC U20  pamoja mchezo wao wa nusu fainal.

Jumatano, 11 Machi 2015

KOCHA ADOLFU RICHARD ASITISHIWA MKATABA WAKE NA TIMU YA POLISI MORO.

Uwongozi wa timu ya soka ya Polisi Moro ya mkoani morogoro inayo shiriki ligi kuu tanzania bara, leo imemsitishia rasmi mkataba wake aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo ADOLFU RICHARD.Akizungumzia suala hilo kocha Adolfu alisema" amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makuwa na amekubaliana na maamuzi hayo kwa faida ya timu na jambo ambalo lilikuwa ndani ya mkataba wake na timu hiyo.Alisema sababu kubwa iliyo mfanya kocha huyo kusitishiwa mkataba wake ni kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michezo yake ya hivi karibuni baada ya timu ya Polisi moro kufungwa na timu ya Simba 1-0, kufungwa na Kagera sukari 2-1, na kufungwa na Mtibwa sukari bao 2-1 pamoja na kutoa suluu ya bila kufungana na timu ya Ruvu shooting katika uwanja wa jamuhuri morogoro".Baada ya matokeo hayo uwongozi  wa timu ya Polisi Moro ulimtaka kocha huyo kutoa maelezo juu ya matokeo hayo na ndipo ulipo amua kutoa maamuzi ya kumsitishia kocha huyo mkataba wake.
Kwa sasa timu hiyo inashikiriwa na kocha wake msaidizi JOHN TAMBA ikiwa na point 20.